Yaliyojiri kwenye Harusi ya Erick Brighton wa Praise Power Radio.

Siku ya Juzi Jumapili ilikuwa ni siku ya Furaha kwa Erick Brighton wa Praise Power Radio na Mkewe, baada ya kufunga Ndoa na Kuunganishwa kuwa Mwili mmoja. Ndoa ilifungwa katika Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God na Kufuatiwa na Tafrija ya Kuwapongeza Maharusi hao iliyofanyika katika Ukumbi wa Banora-Mlimani City. Mc wa Shughuli hii alikuwa ni Mzee wa Gospel Music ya Channel Ten, Boniphace Magupa. Tazama jinsi mambo yalivyokuwa pale ukumbini………

Erick na Mkewe

High Table ya familia ya Erick Brighton

Baba Mzazi wa Erick Brighton

Mama Mzazi wa Bibi Harusi

Kuhoto ni Mdogo wa Erick Brighton

Martha Mwaipaja akiwa na Mumewe

Mc Boniphace Magupa akiwa na Jessica Honore

Mambo ya Mlo hayoooo!!!

Wafanyakazi wa Praise Power Radio wakipata Picha ya Pamoja

Baadhi ya Wadau waliofika kushuhudia Harusi hiyo

Baadhi ya Wanakamati ya Maandalizi. Sailas Kushoto na Mwenyekiti Noel Tenga

Kamati ya Maandalizi ya Harusi ikipata Picha ya Pamoja na Maharusi

Picha ni Kwa Hisani ya Uncle Jimmy
BLOG HII INAWATAKIA MAISHA MEMA NA YA FURAHA, KATIKA MAISHA MAPYA MLIYOANZA!!!

By Gospel News Media Posted in Matukio

Askofu Rodrick Mbwambo: Wajibu wa Mtu aliyeokoka.

Askofu Rodrick Mbwambo



Utangulizi:

Kutokana na wingi wa watu walioko duniani kwa sasa pamoja na bidii ya kanisa katika kutumia tekinolojia mpya za mawasiliano kuwafikishia wenye dhambi injili, ni wazi ulimwengu tulio nao, una idadi kubwa ya waamini kuliko nyakati zilizotangulia katika historia ya kanisa. Hata hivyo, uwingi huu, bado hauendani na hali halisi ya idadi ya watu walioko duniani na uwezo wa kanisa katika kuwafikia wenye dhambi. Dunia kwa sasa ina watu zaidi ya bilioni sita na wakati huo huo, wafuasi wa kweli wa Kristo wakiwa pungufu ya milioni 500.

Tunapoiangalia idadi hii, tunaweza kuona kuwa haiendani kabisa na nguvu kazi iliyopo ndani ya kanisa inayojumuisha watu, uwezo wa kifedha, ufahamu na vitendea kazi. Kutofautiana huku kunaonyesha wazi kuwa kuna kasoro ya kitabia na utendaji kwa waamini wa kanisa la siku za mwisho. Kasoro hii inaonyesha kuwa, wengi wa waamini wako ndani ya wokovu ila hawafahamu wajibu walio nao ndani na nje ya kanisa la Kristo. Ili kulipunguza tatizo hili au kulimaliza waamini kama mwili wa Kristo, wanatakiwa waelewe kwa kina kile wanachotakiwa kukifanya ndani na nje ya kanisa baada ya kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yao.

Huduma za msingi zinazopaswa kufanywa na waamini ni pamoja na hizi yafuatayo:-

KUOMBEA VIONGOZI WA SERIKALI

“Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani; zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni nzuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.” 1 Timotheo 2:1-4

Wajibu wa kwanza unaopaswa kufanywa na waamini baada ya kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao, ni huu wa kuombea viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali. Maombezi haya yahusishe uongozi wa serikali za mataifa yaliyo na nguvu za kiuchumi na kijeshi kuliko mengine chini ya jua. Kwa mfano, bajeti za mataifa mengi yaliyo chini kiuchumi, yanategemea kwa kiwango kikubwa misaada ya mataifa haya yaliyo na nguvu kiuchumi. Kutokana na ukweli huu, kama uongozi wa serikali za mataifa makubwa utayumba, uchumi wa mataifa machanga utayumba pia.

Katika andiko letu hapo juu, mtume Paulo anamwagiza Timotheo kuwafundisha waamini kuwatanguliza viongozi wa serikali mbalimbali katika maombi, kwa kutumia neno ‘kabla ya mambo yote.’ Neno kabla ya yote hapa, ni sawa na kusema, kabla ya kujiombea au kabla ya kuwaombea wengine, ombea kwanza viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali. Kama nilivyotangulia kusema, maombi haya yaguse ulimwengu mzima, ukianzia na viongozi wa serikali ya nchi yako, serikali za mataifa yanayoizunguka nchi yako, bara lako na ulimwengu kwa ujumla.

KUOMBEA VIONGOZI WA KANISA

“Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.” Matendo 12:5

Kama vile wazazi walivyo wa thamani katika maisha ya watoto wa kimwili, viongozi wa kanisa (la kiulimwengu na lile la mahali) nao, ni wa muhimu sana katika maisha ya waamini. Viongozi hawa ndio wanaoandaa na kuratibu malezi ya waamini kuanzia hatua ya uchanga hadi kukomaa kwao. Hali kadhalika, viongozi hawa kwa kiwango kikubwa ndio wanaosababisha baraka za kiroho na za kimwili za waamini. Kutokana na nafasi ya viongozi katika kanisa la Kristo, kila mwamini anatakiwa kuwa na bidii kuwaombea. Kwa kuwa kila mwamini amepandikizwa katika kanisa fulani la mahali, wajibu huu wa kuwaombea viongozi unatakiwa uanzie Yerusalemu ambayo ni kanisa lake la mahali.

Katika andiko letu hapo juu, tunaona kuwa waamini wa kanisa la kwanza walikuwa kielelezo kizuri katika hili. Wao walitambua kuwa, kama adui ataelekeza mshale mmoja kwa mwamini wa kawaida, kwa kiongozi ataelekeza mishale saba. Kwa kulielewa hili, walijijengea tabia ya kuwaombea viongozi wao kwa bidii. Umuhimu wa kuwaombea viongozi umeelezewa pia katika nyaraka mbalimbali zilizoandikwa na Mitume. Mara kwa mara katika nyaraka hizo, neno la Mungu linawakumbusha waamini kuweka bidii katika kuwaombea viongozi katika kanisa. 2Timotheo2:1-2, 1Thesalonike 5:25; 3:1, Waebrania 13:18, Yakobo 5:16. Waamini wasipoelewa umuhimu wa kuuombea uongozi unaowatunza, Ibilisi atapata nafasi ya kuushambulia uongozi huo na kuharibu malezi yao.

Kuhusiana na kile kinachoweza kutokea pale waamini wanapowaombea viongozi wao, nina mfano halisi unaohusu muujiza ulionitokea nilipokuwa nikirejea nyumbani, baada ya kukamilisha huduma katika kijiji kimoja cha mkoa wa Pwani, mwaka 2005. Kabla ya safiri hiyo, mama mmoja katika kanisa alihimizwa na Roho wa Mungu kuniombea. Wakati wa kurejea nyumbani, ‘boneti’ ya gari nililokuwa nikiliendesha ilifunguka na kufunika kioo cha mbele. Kwa kuwa ulikuwa usiku wenye mvua kali, gari iliserereka huku na huko na kimiujiza likasimama tena barabarani! Jambo la kumshukuru Mungu ni kuwa, wakati huu wa kuserereka, hakukuwa na gari lolote lililopita katika barabara ile. Wakati wa kushuhudia kisa hiki kanisani, Roho Mtakatifu alikumkumbusha yule mama juu ya maombi aliyoyafanya kwa ajili yangu!

Kama wewe u mwamini ila ulikuwa hujaona umuhimu wa kuwaombea viongozi wa kanisa, unatakiwa kuanza kufanya hivyo kwa bidii. Anza kwa kuwaombea viongozi wa kanisa linalohusika kukulisha na kukulea kiroho na kisha gusa viongozi wa sharika zingine katika mwili wa Kristo. Taja katika maombi yako viongozi wa kanisa katika mabara ya Ulaya, Asia, Afrika, Amerika Kaskazini na Kusini na Australia na Newzeland. Ukizembea katika hili, utapoteza baraka za Mungu katika maisha yako ya kiroho na yale ya kimwili.

KUTEGEMEZA VIONGOZI

Sambamba na kuwaombea viongozi wa kanisa, waamini wanao wajibu wa kutegemeza viongozi wa kanisa kihali na mali. Kama tulivyoona katika kipengele cha kuombea uongozi, kutegemeza viongozi kunatakiwa kuanzie kwa kanisa la mahali na baadaye kusambae kwa viongozi wa kanisa wa mabara yote. Ni kweli katika makanisa mengi viongozi wanapewa posho, ila posho hii ya kijumuiya hailengi kumzuia mwamini kutoa msaada wa kibinafsi. Misaada ya kimwili inayoweza kutolewa na waamini kwa viongozi wao ni pamoja na chakula, mavazi, nguvu kazi, ujuzi, pesa na kadhalika. Kama kanisa lina viongozi zaidi ya mmoja, ni busara kuwabariki viongozi hao kupitia kwa kiongozi wao. Msaada unaotolewa unaweza kupelekwa kwa mchungaji kiongozi ukiwa na maelezo ya kule unakotakiwa kwenda.

Waamini wanapokuwa na moyo wa kuwategemeza viongozi wa kanisa lao la mahali, ni wazi watakuwa tayari kukutana na mahitaji ya watumishi wengine katika sharika nyingine. Katika kuwategemeza viongozi, waamini wafundishwe kutoipigia panda misaada yao pale wanapoitoa. Kwa mfano kama mwamini amempatia kiongozi shati, asiwatangazie wengine pale atakapomwona kiongozi huyo akiwa amelivaa shati hilo. Kiongozi peke yake ndiye anayeruhusiwa kutangaza zawadi aliyopewa na yule aliyempatia zawadi hiyo. Kama kiongozi ataamua kutangaza zawadi aliyopewa, naye afanye hivyo kwa hekima ili kukwepa kuifungulia mlango roho ya uroho katika maisha yake. Kamwe asitangaze alichopewa ili kuwahamasisha wengine, ila afanye hivyo kuonyesha shukrani yake kwa yule aliyetoa pamoja na kumtia moyo.

MWAMINI AULINDE MWILI WA KRISTO

“…Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.” 1 Wakorintho 12:12-27

Wajibu mwingine wa waamini, ni huu wa kulilinda kanisa la Mungu. Katika andiko letu hapo juu, mtume Paulo anawataka waamini watambue kuwa, wao ni viungo vya mwili wa Kristo, hivyo ndani ya kanisa wako waamini wanaofanya kazi kama mikono, miguu, kucha, vidole, macho, pua na kadhalika. Kwa kuwa viungo vyote vya mwili vinashiriki maumivu pale kiungo kimoja kinapoumia, waamini nao ni wanatakiwa wawe tayari kushiriki taabu za waamini wengine na kuwalinda. Kuhusiana na ulinzi huu, ni vema kila mwamini ahakikishe kuwa anakuwa kinyume na kitu au hali yoyote ile iliyo na shabaha ya kumletea mwingine madhara. Katika hili, waamini wanatakiwa wafuate nyayo za waamini katika siku za kwanza za kanisa kwa kufunua mipango mibaya iliyoelekezwa kwa ndugu zao, kabla ya kuleta madhara. Matendo 9:24; 23:12-24.

Sambamba na waamini kulindana wao kwa wao, wanatakiwa wazidishe ulinzi kwa kiongozi wa huduma au wa kanisa wanalotumika nalo. Kutokana na kuongezeka kwa harakati za adui za kutaka kuwaangamiza viongozi wa kanisa, waamini wawe radhi kujitolea kuyalinda makazi ya viongozi wao mchana na usiku.

KUFANYA KAZI ZA MIKONO KANISANI

Katika ushirika kuna kazi nyingi zinazohitaji nguvu au ujuzi wa kimwili katika kuzifanya. Kazi hizi zinaweza kufanywa na waamini kwa kujitolea badala ya kufanywa kwa pesa. Kazi hizi ni pamoja na uchoraji wa ramani za majengo, kujenga majengo ya ushirika, kupandikiza maua, usafi, kupanga viti kabla ya ibada, kufuta vumbi katika viti vya kukalia ibadani, kujenga majukwaa ya mikutano, kupika wakati wa mikutano, ulinzi na kadhalika. Waamini wafanye hivi kwa furaha wakijua kuwa, kuna baraka zisizo na kifani katika kufanya hivyo. Hata kama itabidi malipo fulani yafanyike, malipo hayo yachukue mwelekeo wa shukrani badala ya mshahara.

Kama waamini watapungukiwa na roho ya kujitolea katika nyumba ya Mungu, wataanza kuliangalia kanisa kama mahali pa ajira badala ya kuwa mahali pa kujitolea. Katika hili, uko mfano ulio hai wa mwamini niliyekutana naye anayetambua umuhimu wa kujitolea katika mambo yanayouhusu ufalme wa Mungu. Niliutambua moyo wake pale nilipomwomba kulitengeneza gari langu baada ya gari hilo kuharibika. Baada ya matengenezo yaliyodumu kwa takribani siku moja, nilimpa kiasi cha pesa nilichodhania kuwa kinalingana na kazi aliyoifanya. Baada ya kuzihesabu pesa nilizompa, alinirudishia sehemu ya pesa zile huku, akisema, “Mchungaji, mbona unanipa pesa zote hizi?!!!” Kama kanisa la Kristo litakuwa na waamini wa jinsi hii, ni wazi mamilioni ya mapesa yanayotumika kama malipo, yataweza kutumiwa kuwategemeza watumishi wanaofanya kazi katika mazingira magumu pamoja na kusaidia huduma zingine za kijamii.

WAJIBU WA KUSAIDIA MASKINI

“Lakini neno moja walitutakia, tuwakumbuke maskini, nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.” Wagalatia 2:10

Ukiangalia neno maskini kama linavyoonekana katika andiko hili, utaona kuwa linamwakilisha mtu yeyote yule asiyejiweza kiuchumi. Kutojiweza huku kunaweza kutokana na kukumbwa na majanga ya kiasili, magonjwa, ulemavu wa viungo, vita, kufiwa na kadhalika. Katika nchi nyingi zilizo nyuma kiustarabu, watu wengi huamini kuwa swala la kuwasaidia maskini, ni jukumu la serikali au mataifa yaliyo na nguvu kiuchumi. Dhana hii kwa kiwango kikubwa inachangia hali ya uwingi wa ombaomba katika mitaa ya nchi hizi.

Tatizo la ombaomba mitaani linaweza kupungua pale wawakilishi wa Mungu (waamini) watakapojivika tabia ya kuwasaidia maskini. Misaada kwa maskini inaweza kupelekwa katika idara za kanisa zinazoshughulikia maskini au katika huduma zinazosaidia maskini zilizo nje ya kanisa.

WAJIBU WA KUFANYA MAOMBEZI

“Wanafunzi wake, Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; kama Eliya naye alivyofanya? Akawageukia, akawakanya. Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo. Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Luka 9:54-56

Andiko letu hapo juu linaonyesha hali halisi inayotawala katika kanisa la siku hizi za mwisho. Leo hii badala ya waamini kuwaangalia wenye dhambi na kuwahurumia, hukimbilia kumwomba Mungu ili ashushe hasira zake juu yao. Wana wa ngurumo walipoomba kibali cha kushusha moto wa hukumu, Yesu alikataa kutoa kibali hicho. Wakati wafuasi wa dini zingine wanapoogopwa kutokana na wepesi wao katika kumwaga damu za watu walio kinyume nao, Wakristo ni lazima waheshimike kutokana na bidii yao katika kufuta machozi ya waliao! Jibu la Yesu kwa wanafunzi wake linaonyesha umuhimu uliopo wa waamini kusimama katikati ya wenye dhambi na Mungu kwa lengo la kuponya. Katika kuishi chini ya jua waamini watakutana na mambo mengi yasiyopendeza ndani na nje ya kanisa, ila katikati ya ubaya huu, zinahitajika rehema badala ya moto uangamizao. Kila mara waamini wanatakiwa kumwomba Mungu ili awasamehe wenye dhambi na kuwarehemu.

Maombezi haya yahusishe pia kuwaombea wale wote wanaojishughulisha katika kuifanya kazi ya Mungu katika mataifa mbalimbali. Katika hili nafasi ya kwanza itolewe kwa wale wanaomtumikia Mungu katika maeneo ambako mwili wa Kristo (kanisa) unaendelea kuteseka.

MWAMINI AMEITIWA KUFANYA UFUASI

“Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa…lakini Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo, na alipomwona, alimhurumia, akakaribia, akamfunga jeraha zake, akazitia mafuta na divai, akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.” Luka 10:30-35

Andiko hili linazungumzia juu ya wema uliofanywa na Msamaria kwa mtu aliyeangukia mikononi mwa majambazi. Tunapofuatilia kisa hiki, tunaweza kuona vile mambo yalivyobadilika pale Msamaria huyu, alipomfikia mhitaji na kumpa msaada. Tukioanisha andiko hili na maisha mapya ndani ya Kristo, tunaweza kuona kuwa, mwamini yeyote yule kabla ya kumpokea Yesu, kwa njia moja au nyingine alikuwa kama huyu ndugu aliyekuwa ameangukia mikononi mwa wanyang’anyi. Ni pale tu yule aliyemwongoza kwa Bwana alipomjia, ndipo hali na mwelekeo wake vilipobadilika. Hapo awali alikuwa anaelekea Kuzimu ila baada ya kukubali kuokoka, maungamo yake yalimpatia haki ya kufanyika mtoto wa Mungu. Yohana 1:12.

Mwamini aliyetendewa wema na mwingine kwa kuonyeshwa nuru ya injili, anatakiwa awe na utayari wa kuwatendea wengine mema. Wakati fulani mtu mmoja alitamka kuwa, kufanya ufuasi ni mapigo ya moyo wa Mungu ndani ya kanisa, hivyo kanisa (mwamini) lisilo na bidii ya kuwaleta wengine kwa Bwana limekufa.

KUITEGEMEZA KAZI YA MUNGU

Huduma nyingine inayotakiwa kufanywa na waamini, ni hii ya kuitegemeza kazi ya Mungu kifedha. Katika hili waamini wanatakiwa kufahamu kuwa, katika ufalme wa Mungu hakuna huduma iliyo na mtu maalum wa kuifanya. Baadhi ya waamini wanaweza kuwa mstari wa mbele katika kutegemeza huduma fulani, ila hali hiyo haiwaondolei wengine nafasi ya kushiriki katika kutoa walicho nacho ili kuitegemeza huduma hiyo. Waamini wasipoujua ukweli huu, watafanya makosa ya kuuangalia ushirika kama ushirika wa watu fulani.

Mwamini anapouchukulia ushirika kama mali yake, atafanya kila analoweza kuutegemeza ushirika badala ya kungojea mwingine afanye. Kama ushirika utakuwa na hitaji la kupata kiwanja, jengo, vifaa vya muziki, usafiri, majengo ya shule, posho za watumishi, kulipia huduma za simu, umeme, tovuti, vipindi redioni na kadhalika, atajiweka mstari wa mbele kutoa ili kugharimia huduma inayotakiwa.Tukikutana siku nyingine tutaongea huduma nyingine zinazopaswa kufanywa na waamini, ila kabla ya wakati huo nakuacha na amani ya Bwana. Ameni

Na: Askofu Rodrick Mbwambo

By Gospel News Media Posted in Matukio

Bahati Bukuku asindikiza vyema Tamasha la Marafiki ndani ya CCM Kirumba, chini ya Living Water Fm.

Jana ilikuwa ni Siku ya lile Tamasha kubwa kabisa la Marafiki lililofanyika katika Kiwanja cha CCM Kirumba kuanzia mida ya Saa 8 – Saa 1 usiku. Tamasha hili liliandaliwa na Kituo cha Radio ya Kikristo ya Jijini Mwanza Living Water Fm kinachorusha Matangazo yake kupitia Masafa ya 103.3Mhz kwa Upande wa Kanda ya Ziwa Victoria.

Mgeni Rasmi katika Tamasha hilo alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Cordial Tours Bw. David Kizito. Ma Mc wa Event hii walikuwa ni Maganga James Gwensaga(Living Water Fm) na Harris Kapiga(Clouds Fm). Udhamini mnono wa Nyanza Bottling Company kupitia kinywaji chao cha Coca Cola, Cordial Tours na Living Water Fm, ulifanikisha kufanyika kwa Tamasha hili.

Muimbaji Mkongwe wa Muziki wa Injili Bahati Bukuku alikuwepo pia katika Tamasha hilo akiwa kama Muimbaji mualikwa toka Nje ya Mwanza. Kwaya, bendi na waimbaji binafsi pia walipata nafasi ya Kutumbuiza katika Tamasha hilo lililokusanya umati wa watu toka Sehemu mbalimbali za Mkoa wa Mwanza ili kujumuika Pamoja kama Marafiki.

Mambo yalikuwa hivi………………………………………

Baadhi ya Watu waliohudhuria Tamasha hilo


Ma Mc wa Event hii……………………………

President Maganga James Gwensaga, ambae pia ni Station Manager wa Living Water Fm

Harris Kapiga toka Clouds Fm


Baadhi ya Kwaya na Bendi zilizotumbuiza ni kama………….

E.A.G.T Msumbiji Choir

Tumaini Anglican Choir

Revival Mission Band

Watoto wa Bishop Isaah Zenobius

Mwisho wa Siku Bahati Bukuku ndo akafunga pazia la Waimbaji kwenye Tamasha hilo

Bahati Bukuku


Na kwasababu lilikuwa ni Tamasha la Marafiki, Watangazaji wa Radio mbalimbali za Injili za Jijini Mwanza pia Walialikwa

Kulia ni Blogger Sowane Emmanuel(Hhc Alive Fm) na Nyamiti Kayora(Star Tv)

By Gospel News Media Posted in Matukio

Living Water Fm na Tamasha la Marafiki ndani ya CCM Kirumba.

Radio ya Kikristo ya Living Water Fm ya Jijini Mwanza inayosikika kupitia Masafa ya 103.3Mhz, imeandaa Tamasha la Marafiki litakalofanyika Siku ya Jumapili Tarehe 27 katika Kiwanja cha CCM Kirumba kuanzia mida ya Saa 9 Jioni na Kuendelea. Mwimbaji mkongwe wa Muziki wa Injili toka Tanzania Bahati Bukuku atakuwepo kusindikiza Tamasha hilo. Viingilio: WAKUBWA 2000 na WATOTO 1000. NJOONI TUJUMUIKE PAMOJA KAMA MARAFIKI KATIKA KRISTO. Tangazo hili limekosewa Tarehe, na Samahani kwa Usumbufu uliojitokeza!!!

By Gospel News Media Posted in Matukio

Patrick Sanga: Jifunze Kumiliki Majibu ya Maombi yako.

Yoshua 13:1-7

Utangulizi,

Katika dunia ya leo watu wengi sana wamekuwa wakitumia muda wao mwingi ikiwa ni pamoja na kufanya maombi ya kufunga na kuomba ili kumuomba Mungu awabariki, awaponye, awalinde kwa kifupi awajibu mahitaji yao waliyonayo mbele zake siku zote. Wapo waliokuwa hawazai wamezaa, vipofu wameona, wasioajiliwa wameajiliwa, biashara za wengi zimefanikiwa, ndoa nyingi Mungu ameziponya, wapo waliotaka kuolewa au kuoa na Mungu amewapa waume na wake wazuri.

Sasa hao hao watu ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika kuomba Mungu awatendee miujiza katika maisha yao, imefika mahali wanaona yale ambayo yalikuwa ni majibu ya Moambi yao shetani ameyavamia na kuleta balaa zaidi na limekuwa pigo kubwa sana kwa wana wa Mungu. Na kwa sababu hiyo wamejikuta wakimlalamikia Mungu kama vile wana wa Israeli na imefika mahali pa wengine kuona kama Mungu hawezi na hivyo kumuacha.

Tatizo la haya yote ni kwamba wakristo wengi hawana tabia ya au mazoea ya kumiliki mujibu ya maombi yao toka kwa Mungu. Huenda ulikuwa huna mtoto na Mungu amekupa kuzaa mtoto, sasa huyo mtoto ndiyo jibu lenyewe kutoka kwa Mungu. Sasa ni lazima ujifunze kumiliki huo muujiza wa mtoto, sasa si mtoto tu bali ni pamoja na ajira, ndoa, uponyaji, kanisa, Nchi, Biashara nk.

Kusudi la waraka huu mfupi ni kukufundisha njia zitakazokusaidia kumiliki majibu ya maombi yako na kukupa maarifa yatakayokusaidia kuwa makini na majibu ya Mungu katika maisha yako.Tafsiri ya Kumiliki, Neno kumiliki linapozungumziwa kibiblia lina maana ya kukiweka kitu au jambo fulani chini ya utawala wako, maana yake unakuwa na nguvu au umri juu ya hicho kitu. Una hakikisha hakiwezi kutoka kwako. Kumiliki siku zote kunahusisha mapambano makali Sasa mimi sijui Mungu amekutendea nini? Ila ninachojua kwa namna moja au nyingine lazima kuna mambo ulikuwa unamuomba Mungu akufanyie na mengine tayari ameshakufanyia na mengine ndiyo anayafanya na bado kuna mengi atafanya.sasa katika hayo aliyokwisha kufanya huenda amekupa mke au mme mtarajiwa, huenda ameiponya ndoa yako, nafsi yako, mwili wako, Afya yako, Huenda amekupa mtaji, amekupandisha cheo, amekupa mtoto, amepanua mipaka ya huduma yako nk.

Katika lolote ambalo amekufanyia unatakiwa kulimiliki kwa maombi. Kama shetani alikuwa hataki uzae usidhani atamfurahia mtoto uliyemzaa. Kama alishindwa kumzuia asizaliwe usidhani atakubali aendelee kuishi. Shetani atafanya kila analoweza kuua huyo mtoto au kuharibu chochote kile ambacho Mungu amekutendea kama jibu. Sasa kwa sababu hiyo ni lazima uzijue njia za Kibiblia zitakazokusaidia kumiliki hayo majibu ya maombi yako kutoka kwa Mungu.

Huenda zipo njia nyingi zifuatazo ni sehemu na ni za msingi kati ya hizo nyingi.

Njia ya kwanza, kumiliki kwa kuupigania na kuujenga huo muujiza au jibu lako toka kwa Mungu.

Yoshua 13:1-7, 2 Samwel 2:1-7.Ule mstari wa kwanza wa kitabu cha Yoshua katika kitabu Yoshua 13 unasema “Basi Yoshua alipokuwa mzee na kuendelea sana miaka yake BWANA akamwambia wewe umekuwa mzee na kuendelea sana miaka yako, kisha inasalia nchi nyingi sana bado kumilikiwa” Kumbuka katika ile sura ya kwanza ya kitabu cha Yoshua Mungu anamwambia Yoshua uwe Hodari na moyo wa ushujaa maana ni wewe utakayewarithisha watu wa nchi hii. Na ukisoma vizuri kitabu chote cha Yoshua unaona kabisa Yoshua alitekeleza agizo la kuwarithisha wana wa Israel nchi ya ahadi.

Wakati Mungu anamwambia Yoshua bado inabaki nchi yaani maeneo mengi sana ambayo bado hayajamilikiwa tayari Yoshua alikuwa ameshapiga zaidi ya wafalme 32 na kuiteka miji yao, lakini bado Mungu anamwambia bado nchi nyingi inasalia. Kitu gani Mungu anataka tujifunze hapa? Sikiliza Yoshua alipewa kuwarithisha wana wa Israel nchi hii lakini sio kuwamilikisha. Suala la kumiliki lilikuwa kwa yule aliyekabidhiwa nchi au mji lakini sio kwa Yoshua. Sasa ndiyo maana Mungu akamwambia Yoshua kwa sababu wewe ni mzee igawanye hiyo nchi kwa wana wa Israeli kwa kufuata kabila zao ili waweze kumiliki. Maana yake waingie kwenye mapambano ya kile ambacho Mungu amewapa kupitia Yoshua.

Niseme hivi chochote unachokipata kwa njia ya maombi kinamilikiwa kwa njia ya maombi, jifunze kukipigania na kukijenga yaani kuendelea kukiri uwepo wa hicho kitu siku zote. Mfano kama uliomba mke au mme na Mungu amekupa usipunguze kuomba maana shetani usidhani anafurahia ndoa au uhusiano wenu. Ukiendelea kusoma zile sura zinazofuata za kitabu cha Yoshua ndipo utakapoona makabila yalivyopambana ili kumiliki jibu lao toka kwa Mungu la nchi.

Njia ya Pili; Miliki majibu yako kwa kutafuta maarifa zaidi ya kutunza huo muujiza.

Hosea 4:6a inasema “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa”.Sikiliza muujiza au jibu lolote lile ambalo Mungu amekujibu au amekutendea una maarifa yake ya kuutunza. Maarifa hayo yanaweza kuwa ndani ya Biblia na hata katika vitabu vingine nje ya Biblia. Mfano umemwomba Mungu akupe mtaji uanze biashara na Mungu amekupa, sasa huo mtaji una namna zake za kuuendesha ili uweze kuzaa kwa faida. Kuna namna fulani ambayo ukiwekeza utapata faida nzuri. Sasa maarifa hayo ya kuwekeza yapo mengine kwenye Biblia lakini mengine ni kupitia watu wenye uzoefu katika hilo eneo, vyombo vya habari, kuna semina za kiserikali kuhusu biashara nenda huko ufuatilie ili ujue zaidi, maana apendaye mafundisho hupenda maarifa. Huenda ulikuwa hujaoa au kuolewa na sasa uko kwenye ndoa. Hudhuria semina za ndoa na kusoma vitabu husika ili upate maarifa yatakauokusaidia kuishi katika ndoa vizuri.

Umezaa watoto wengi wanakufa kwa malaria halafu watu wanasema ni shetani tu wakati mwingine si shetani ila ni wewe ulimweka mwanao katika mazingira ya kuumwa na mbu vizuri ndio maana akafa. Soma habari za matumizi ya ngao, chandarua yanayotolewa na serikali hujui kwamba serikali yoyote ile imewekwa na Mungu. Kwa kifupi muujiza wowote amabo Mungu amekutendea una maarifa yake ya kuutunza na chanzo kikubwa cha maarifa ni neno la Mungu. Hivyo lisome likae kwa wingi ndani yako.

Njia ya Tatu; Miliki majibu yako kupitia shukrani, sadaka au utoaji wa aina yoyote ile.

2Wafalme 5:17”Naamani akasema kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili, kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa BWANA.

Hizi ni habari za Namani Jemedari wa jeshi la shamu alikuwa na Ukoma. Alipokwenda Istraeli kwa nabii Elisha ili aombewe kuhusu tatizo la ugonjwa wake Elisha alimpa maagizo ya kutekeleza kuwa akajichovye / akajizamishe ndani ya mto Yordani mara saba na ndipo atapona. Baada ya Namani kutii maagizo Biblia inasema alipona na ngozi yake ikatakasika ikawa kama ya mtoto mchanga.Baada ya jibu hilo kwanza Namani alimshukuru Mungu wa Elisha na kisha akasema tangu siku ile hatatoa tena sadaka kwa miungu yao kule shamu isipokuwa kwa Mungu wa Elisha pekee.

Unapomshukuru Mungu kwa lile alilokutendea ni ishara ya kupokea kwa kuonyesha kujua nani aliyekutendea hilo jambo na hivyo kumrudishia yeye utukufu. Pia unaweza kumiliki majibu ya maombi yako kwa njia ya kutoa sadaka kwa yatima, wajane na pia unaweza kumshukuru Mungu kwa kushuhudia kwa wengine nini Mungu kakutendea au kutoa sadaka ya shukrani au utoaji kwa makundi mengine yasiyojiweza katika jamii.

Njia ya nne: Kumiliki muujiza kwa kuwatunza watumishi wa Mungu na kuchangia huduma mbalimbali.

Yoshua 12:1-3 kwenye ule mstari wa pili Biblia inasema “Basi wakamwandalia karamu huko naye Martha akamtumikia na Lazaro alikuwa mmoja wapo wa wale walioketi chakulani pamoja nao.

Hii pia ni habari nyingine inamhusu Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua baada ya kuwa amekufa kwa siku nne. Sasa Lazaro aliumiliki muujiza wake wa kufufuliwa kwa kumtunza Yesu pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. Hii ina maana Lazaro pamoja na dada zake waliingia gharama kwa ajili ya kuwatunza Yesu pamoja na wanafunzi wake, Kwa siku zote ambazo Yesu alikaa kwa Lazaro, Lazaro alihakikisha hawalali njaa, anawapa mahali pa kulala nk.

Sasa unaweza kumiliki muujiza wako kwa kuruhusu watumishi wa Mungu wakae nyumbani kwako. Huenda wamekuja kwenye mkutano au semina kwa wiki moja au mbili itoe nyumba yako itumike, kufanya hivyo ni kumfanya Mungu aendelee kukulinda wewe na yale aliyokupa maana anajua hutamnyima siku moja atakapohitaji kuvitumia. Wapo wengine wanaomiliki kwa kutoa magari yatumike kipindi chote cha mikutano, unaweza pia kumiliki kwa kuchangia gharama za mikutano si lazima pesa lakini hata kufanya kazi mbalimbali katika mkutano huo, huenda ni usafi, kubeba vyombo, kufanya usafi walikofika watumishi, kuombea huo mkutano au semina nk. Nakuambia unaweza ukaona kama ni vitu vidogo lakini ndivyo mujibu ya maombi yanavyomilikiwa bila kujali Mungu amekutendea nini.

Nija ya tano: Kumiliki muujiza kwa kufanya maamuzi ya kuokoka endapo Mungu alikufanyia huo muujiza kabla hujaokoka, na kuwaambia wengine habari ya Yesu aliyekuponya.

Ukisoma ile sura nzima ya 9 ya kitabu cha Yohana utakutana na habari ya kipofu mmoja tangu kuzaliwa kwake ambaye Yesu alikuwa amemponya. Ule mstari wa 39 unasema “akasema,Naamini, Bwana akamsujudia” Ukisoma vizuri habari hii utagundua baada ya mahojiano marefu kati ya mafarisayo na yule kijana kuhusu uponyaji wake ndipo Yesu akamwuuliza je unamwamini mwana wa Mungu? Yule kijana akamwuliza ni nani huyo nipate kumwamini? Kwa kifupi Yesu akamjibu unayezungumza naye. Ndipo yule kijana akasema, naamini Bwana akamsujudia.

Mtu mwingine ni Naamani ambaye tumekwisha ona habari zake, kitendo cha yeye kusema toka leo sitatoa sadaka kwa miungu ya shamu ila kwa Bwana ni dalili ya kuonyesha kumwamini Mungu wa Israel. Hivyo hata leo wapo ambao Mungu anawatendea mambo mengi hata kabla hawajaokoka sasa ili kumiliki hayo ambayo Mungu amekufanyia mwamini Yesu ndio huo muujiza utadumu. Wapo watu leo wanafunguliwa kwenye nguvu za mapepo huo ni uponyaji. Sasa badala ya kuwasaidia watu wamwamini Yesu tunawaacha, nakuambia pepo watarudi kwa huyo mtu wenye nguvu zaidi kuliko yule wa kwanza.

Pia ukisoma vizuri habari hiyo hiyo utagundua kwamba huyu jamaa alimiliki uponyaji wake kwa kuwaambia wengine habari za Yesu na kukiri kwamba mponyaji ni Yesu na si mtu mwingine, nakuambia kufanya hivyo ni kujihakikishia kudumu kwa huo muujiza na Mungu ataendelea kuutunza huo muujiza maana wewe ni chombo chake. Mungu akikuponya au kukubariki usinyamaze kimya waambie wengine habari za Yesu aliyekuponya. Jifunze kutoka kwa mwanamke msamaria. Uponyaji wa nafsi yake ulipelekea watu wengi wa mji wa Samaria kuokoka. Soma kile kitabu cha Yohana sura ya nne mistari 30 ya kwanza utaiona habari hii.

Mpenzi msomaji wangu mpaka hapa naamini utakuwa umepata kitu cha kukusaidia labda nikuambie hivi siri kubwa ya mafanikio ni kuliweka neno la Mungu kwenye matendo, si unajua imani pasipo matendo imekwisha kufa katika nafsi ya huyo mtu mwenye imani hiyo. Nimeamua kuandika ujumbe huu baada ya kuona wana wa Mungu wengi imefika mahali wanakuta yale ambayo Mungu aliwapa kama majibu ya maombi yao yameshaharibiwa na shetani, wapo waliozaa watoto wao wakafa na walimuomba sana Mungu kuhusu hao watoto nk. Sasa ni imani yangu kwamba tangu sasa jambo lolote ambalo Mungu atakupa kama jibu la maombi yako utalimiliki.

Na: Patrick Sanga

The genius of Mary Mary

Mary Mary

They have a hit TV show on WEtv and the #1 album on the Billboard Gospel charts. Everything seems to be going pretty well for Mary Mary these days. While they are entertaining us on TV and ministering to us through music, they are subtly teaching and reinforcing a lesson to everyone. What they are doing is pure genius.

Now, when I say Mary Mary, I don’t just simply mean Erica and Tina Campbell. I’m referring to the entire team that makes the Mary Mary machine go. If their TV show has taught us anything, we have learned that there are many people behind the scenes that are responsible for the finished product that we hear on MP3s and see on stage.

We have seen a number of celebrities with their own reality TV show before. Some of them have even been musicians or music industry types. How many of them have had the forethought to release an album during the run of the show? They have even integrated their music into the show. By doing this, they are exposing their music to a completely new audience.

Think about their current album “Go Get It”. Like I said before, it is #1 on the Billboard Gospel charts. The album is also #16 on the Billboard top 200 and #3 on the R&B/Hip-Hop charts. That in of itself may not seem too out of the ordinary to you. However, let’s consider the songs on the album.

There is no denying that “Go Get It” is a hit song. When you look at that other songs on the album, you’ll find that most of them were recored on previous Mary Mary albums. For the most part, these songs aren’t even remixes. They sound like the original recordings.

In a day and age where you can easily buy just one song from without buying the entire album, they’re topping the charts with an album filled with a bunch of previously recorded music. A big factor for this has to be be because they tied the album and the show together. The new audience from the show means that there are people that may not have heard the “old songs”. Therefore people are buying these songs for the first time. This is absolutely brilliant!

There may have been certain factors like pregnancies that prevented them from releasing an album that has more new music. There is a chance that releasing an album full of classics could have been their plan all along. Whatever the original intent was, the end result definitely worked out in their favor.

It is pretty unlikely that we’ll see massive amounts of Gospel artists get reality shows. However, one thing we can all learn from what Mary Mary is doing is to take full advantage of every opportunity that is presented in front of us. When opportunities arise in our lives, we really need to figure out what we can do to maximize them.

By Gospel News Media Posted in Habari