Gospel News Media

Taking Gospel To The Next Level!

  • About Us
  • Contact Us
  • Join Our Prayer Line
  • Prayers To Accept Jesus
  • Ratiba Ya Vipindi – Hhc Alive Fm
  • Shuhuda

Kuhama kwa Blog Hii.

Posted by Gospel News Media on September 7, 2012
Posted in: Matangazo. Leave a comment

Blog hii sasa imehama. Unaweza kutembelea blog hii kupitia Tovuti ya; http://www.gospelnewsmedia.org

Kwa kuitembelea Tovuti hii hivi sasa,Bofya Hapa

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

Watumie rafiki zako kupitia;

  • Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Share on X (Opens in new window) X
  • Share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Email a link to a friend (Opens in new window) Email
Like Loading...

Mchungaji Kanisa la Gospel Campaign Centre, Azindua Operation maalum ya wiki tano ya Maombezi na Uponyaji.

Posted by Gospel News Media on August 27, 2012
Posted in: Habari. 1 Comment

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Gospel Campaign Centre, la Majumbasita UkongaJijijini Dar es salaam, Moses Magembe, amezindua kampeni maalumu ya maombi na maombezi, kwa muda wa majuma matano, ambapo kazi ya kuwafungua na uponyaji unaoambatana na matendo makuu ya nguvu za Mungu  utaanza rasmi.

Akiongea katika Ibada ya  hiyo maalum alisema  kazi ambayo ameianza haitazimwa bali ameamua kuwasha moto katika siku za Jumatano,Alhamisi,Ijumaa na Jumapili kwa muda wa majuma yote matano fulululizo, hivyo ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na Vitongoji vyake, wakiwepo watu kutoka mikoa mbalimbali, kujitokeza kwa wingi kuhudhuria maombezi hayo muhimu kwani katika kanisa hilo, masuala ya miujiza siyo kitu cha kushangaza bali watu wamekuwa wakitendewa na Mungu pasipo shaka.

Watu wengi walifunguliwa kupitia Ibada hiyo ya kipekee mara baada ya kuombewa na mpakwa mafuta wa huyo wa Bwana, Mchungaji Moses Magembe ambaye ameamua kujitoa mhanga, kuieleza kweli mbele ya jamii ya Wakristo, na kuipinga imani potofu zilizozagaa nchini, huku akiamua kuendesha Operation maalumu, ya maombezi kupitia jina kuu la BWANA Yesu Kristo.

Watumie rafiki zako kupitia;

  • Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Share on X (Opens in new window) X
  • Share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Email a link to a friend (Opens in new window) Email
Like Loading...

The Holy Bass Guitar Concert with James Honore in Dar es saalam.

Posted by Gospel News Media on August 23, 2012
Posted in: Matangazo. Leave a comment

Watumie rafiki zako kupitia;

  • Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Share on X (Opens in new window) X
  • Share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Email a link to a friend (Opens in new window) Email
Like Loading...

Faustin Munishi kuhubiri Injili Nchini Congo Mwezi huu.

Posted by Gospel News Media on August 23, 2012
Posted in: Habari. Leave a comment

Mtumishi wa Mungu Nabii na mwimbaji wa nyimbo za injili Faustin Munishi kuzuru GOMA Nchini CONGO DRC leo kwa ziara ya siku tatu ya kiutumishi.

Mtumishi Munishi anatarajiwa kuondoka uwanja wa Jomo Kenyatta airport mida ya saa tatu asubuhi leo na ndege ya Rwanda Air.

Munishi anatarajia Kuhubiri Injili Nchini Congo katika mji wa Goma
sehemu ijulikanayo kama Cadeco Birere. Mkutano huo utaanza tarehe 27 mwezi huu wa 8.

Hapa Munishi anasema “YESU ANAIWEZA GOMA. Atawasamehe wote watakaotubu. Atawaponya wagonjwa wote watakaoamini kwa nguvu yake ya uponyaji. Atayabadilisha Maisha ya wote watakaolikubali Neno lake. Amen”

Nyote Mnakaribishwa

Watumie rafiki zako kupitia;

  • Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Share on X (Opens in new window) X
  • Share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Email a link to a friend (Opens in new window) Email
Like Loading...

SIMULIZI: Nilikula Nyama za ndugu zangu wa damu 19 (Sehemu ya Nne).

Posted by Gospel News Media on August 21, 2012
Posted in: Simulizi. Leave a comment
Inaendelea………………………………………….
Nilifikiria sana kwa wakati ule, na kabla sijapata jibu nikakuta machozi yanaanza kunitoka. Nilifikiria sana kuhusu swala hili. “Yani ndugu yangu wa damu? Kisha! Auliwe na kuliwa? Niliwaza mwenyewe kichwani mwangu na gafla nikajikuta natoa sauti kubwa kwa kusema “Hapana kwakweli.” Haikuchukua muda mrefu kiongozi yule wa wachawi kaagiza wachawi wengine wawili kunipeleka kwenye chumba flani hivi. Wachawi wale walikuwa ni wanaume. haraka haraka wakanichukua mpaka kwenye kile chumba.

Kilikuwa ni chumba kilichokuwa kimejaa giza sana, jambo nililoweza kuliona kwa haraka ulikuwa ni moto uliokuwa ukiwaka kwa mbali kidogo toka sehemu ile tulipokuwa tumesimama. Bado tulikuwa kwenye chumba kili kile mana ni kirefu sana. Wakanisogeza mpaka karibu na ule moto.

Sikuamini kitu nlichokuwa nakiona mbele ya Macho yangu kwa wakati ule. Machozi yalizidi kunitiririka kwa nilichokuwa nikikiona mbele yangu. Ilikuwa ni sehemu ambayo imetengenezwa kama sehemu ya kuchomea mishikaki hivi, chini kulikuwa na moto mkali sana ukiwaka na juu ya moto kulikuwa na bati flani hivi ambalo liliwekwa vitoto vichanga sana, ambavyo huwa vinatolewa tumboni mwa mama zao angali mama zao ni wajawazito.

Maskini ya Mungu vitoto vile vilikuwa vikichomwa moto na kadri zilivyokuwa vikiyeyuka mafuta yale yalikuwa yakiingia moja kwa moja kwenye bakuli 1 kubwa sana. Mmoja wa waachawi wale wawili alienda moja kwa moja kwenye moja ya bakuli liliokuwa likitumiwa kuhifadhia mafuta yale. Alichukua mafuta kidogo akachanganya na dawa flan zilizokuwa pembeni ya lile bakuli na kuanza kuninyunyizia usoni huku wakiimba wimbo ambao mi sikuweza kuutambua.

Baada ya kama dakika 5 hivi, nikajikuta nimekuwa mtu wa tofauti sana. Gafla nikawa jasiri, mtu nisiyekuwa mwoga. Nilijawa na roho ya unyama kiasi cha kutokuona huruma ya viumbe walw wadogo waliokuwa wakichomwa moto. Kwa wakati huu niliona ni jambo la kawaida sana kwa kitendo kile.

Baada ya wachawi wale kuridhika na hali niliyokuwa nayo kwa sasaiv, walinirudisha kwenye kikao kile na kunikalisha karibu na kiongozi wao. “Sasa unaweza kuzungumza, endelea sasa” Hiyo ndo ilikuwa kauli ya kwanza ya kiongozi yule wa wachawi baada ya mimi kukaa chini.

Kwa wakati huu sikuchukua muda sana kufikiria kwani niliona ni jambo la kawaida tu kula nyama ya mtu. Nilitumia kama sekunde kadhaa hivi na kutoa jibu “Baba yangu”.

NINI KITAENDELEA? JE! NI KWELI BABA YAKE MZAZI EA ESTHER ATAULIWA NA WACHAWI NA KULIWA? NA JE! UJASIRI ALIONAO HIVI SASA ESTHER NI WA MUDA TU AU NI WA KUDUMU?

Kwa Muendelezo wa Simulizi hii, Bofya Hapa

Watumie rafiki zako kupitia;

  • Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Share on X (Opens in new window) X
  • Share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Email a link to a friend (Opens in new window) Email
Like Loading...

Kanisa la EAGT Tarime ladaiwa kuuziwa Kiwanja cha Serikali kinyemela.

Posted by Gospel News Media on August 18, 2012
Posted in: Habari. Leave a comment
MAMLAKA ya Mji mdogo Tarime imeunda kamati ndogo  kwa ajili ya kuchunguza eneo la wazi  la Serikali lililoko kitongoji cha Mwangaza kata ya Nyamisangura Wilayani Tarime lililodaiwa kuuzwa na wataalamu wa mipango miji na ardhi wa mamlaka ya mji mdogo  kwa kanisa la  EAGT Tarime.
 Uamuzi huo wa kuundwa kwa kamati ndogo umekuja baada ya kudaiwa kuwa kuna uwanja  wa wazi uliotengwa na Serikali kwa ajili ya kujengwa Zahanati na shule ya awali lakini matokeo yake wataalamu wa ardhi wa mipango miji wameuza eneo hilo la wazi kwa kanisa la EAGT.
 Wajumbe wa Baraza la mamlaka hiyo walisema kuwa wameshangazwa kwa kitendo cha wataalamu kuuza eneo la Serikali kwa kanisa  huku wakijua  eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya Shule na Zahanati.
 “Mwaka  1998 nikiwa Mwenyekiti wa eneo la Mwangaza, Serikali ilitenga eneo  la wazi kwa ajili ya kujengwa shule na zahanati. Serikali ikatoa fidia  kwa watu na wakahamishwa kupisha eneo hilo. Leo hii wataalamu wa mipango miji na ardhi wamepima eneo wanasema ni la kanisa!”
 Aliongeza ”Ndugu Mwenyekiti tunaomba kamati ndogo iundwe kuchunguza swala hili, hapa kuna jambo limejificha kuna rushwa imetumika na isitoshe nina nyaraka za watu waliolipwa fidia na Serikali tofauti inavyoelezwa sasa kuwa kanisa la EAGT ndilo limelipa wananchi fidia  kupisha eneo” Alisema mwenyekiti wa kitongoji cha Ronsoti Chacha Kisanta.
 Ofisa mipango miji wa mamlaka ya mji mdogo Tarime Nzengula Wilfred alisema kuwa  eneo hilo ni la Kanisa la EAGT , na kuwa taratibu zote zilifuatwa kutoka kwa kamishna  wa Ardhi na kwamba tatizo la ufahamu mdogo wa wajumbe kuhusu maswala ya ardhi ndiyo chanzo cha kuibua migogoro.
 Hata hivyo maelezo ya Ofisa mipango miji yaliwakwaza wajumbe ambapo walimtaka ofisa huyo kufuta kauli yake kwa kile alichodai kuwa wajumbe wana uwelewa mdogo kuhusu ardhi.
 Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwangaza Joseph Maseke  na wajumbe wengine wakaomba watafutwe watu waliolipwa fidia na Serikali mwaka 1998 ili kuthibitisha  kwakuwa wapo hai kutokana na madai ya kanisa la EAGT kudai kuwa wao ndio waliolipa fidia wananchi.
 “Tuna akili timamu! sisi si wajinga. Uzuri watu waliolipwa fidia wapo hai tuwatafute watupe hali halisi tujue ni taratibu zipi zilitumika  hadi kanisa likamilikishwa  eneo la wazi kwani tumekuwa tukiona wataalamu wakifika kwenye maeneo wanapima bila hata kuwahusisha wenyeviti wa vitongoji, na mitaa na hili tatizo ni kwasababu maeneo mengi hayana hati miliki basi hilo kanisa lingejenga shule au zahanati kama ilivyokuwa kipaumbele cha Serikali!” Alisema Maseke.
 Hali hiyo ya wajumbe  wote kuwalalamikia wataalamu kwa kuuza eneo la Serikali na kuomba iundwe kamati ndogo ya uchunguzi, Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo Tarime Christopher Mantago alichagua kamati ndogo ya wajumbe 6 watakaofanya uchunguzi kati yao 3 wanatokea eneo la Ronsoti na mwangaza,wajumbe wawili kutoka mamlaka ya mji mdogo na mmoja kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Dinna Maningo – Tarime.

Watumie rafiki zako kupitia;

  • Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Share on X (Opens in new window) X
  • Share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Email a link to a friend (Opens in new window) Email
Like Loading...

Mwl. Christopher Mwakasege; Zijue Karama Za Roho Mtakatifu – II

Posted by Gospel News Media on August 18, 2012
Posted in: Mafundisho. 4 Comments

Mwl. Christopher Mwakasege

SEHEMU YA NNE
Karama ya neno la Maarifa
I Wakorintho 12:4,8; ”Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima, na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule”.
Kama tulivyo jifunza huko nyuma kazi ya karama ni kulijenga kanisa.
Kazi ya karama ya neno la maarifa.

 Kukupa habari ya mambo yaliyopo na/au yaliyopita ili kukurahisishia kufanya maamuzi na kutambua hila zilizojificha ili kukwamisha utumishi wako.

Wakati mwingine karama hii itakupa kujua maswali waliyonayo watu kabla hawajauliza au kujua mahitaji waliyonayo kabla hawajakwambia.
Njia nne ambazo karama ya neno la maarifa inafanya kazi:
i. kwa kutumia mawazo
ii. kwa kutumia ndoto
iii. kwa kutumia maono, maono yamegawanyika katika sehemu zifatazo:

 maono ya ndani

 maono ya wazi

 maono yanayotokea wakati akili zako hazina matunda.(suspended)
iv.  kwa kutumia njia ya kuweka mwilini mwako maumivu au hali aliyo nayo mtu mwenye kuhitaji.

Karama zinafanya kazi kwa kutegemeana/kushirikiana.
Mfano. Unaweza kupewa swali na jibu. Kulijua swali ni neno la maarifa na kujua jibu la swali hilo ni neno la hekima.

i. Njia ya kutumia MAWAZO / WAZO
Hii ndio njia kuu ambayo inatumika mara nyingi zaidi. Marko 2:6-8 inasema ”……. Mara (ghafla) Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao…..”. Maana yake ghafla wazo tofauti, na lile alilokuwa akiwaza saa hiyo lililetwa na Roho Mtakatifu ndani yake.
Ukisoma Luka 3:15-16; inasema ”……….Yohana alijibu akawaambia wote,…………”. Yaani alijibu swali ambalo lililetwa ndani yake na Roho Mtakatifu; sio kwamba aliulizwa na mtu yeyote yule.
Luka 20:18-26; inasema ”……….wakamvizia-vizia, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wamnase katika maneno yake, wapate kumtia katika enzi na mamlaka ya liwali. Wakamwuliza wakisema,………………. Lakini yeye alitambua hila yao akawaambia ……………. Wakastaajabia majibu yake, wakanyamaa”.

Mambo ya kukuwezesha kufanya kazi na njia hii ya mawazo:
a. Jizoeze kukabidhi roho yako, nafsi yako na mwili wako kila siku upya mbele za Mungu.
b. Omba maombi ya vitu vifuatavyo:

 Usikivu (sensitivity)

 Utulivu

 Kufundishwa na Mungu namna ya kutembea katika hiyo karama.
Hii inasaidia kwa mfano, Mungu akisema jenga safina wakati sio msimu wa mvua. Yaani kutii sauti ya Mungu bila kuangalia dalili za nje.

SEHEMU YA TANO
Karama ya neno la hekima

I Wakorintho 12:4,8; inasema ” Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima…….”.
I Wakorintho 14:12 ” ……takeni sana mzidi kuwa nazo ili kulijenga kanisa”.
Karama ya neno la maarifa na neno la hekima zinafanya kazi kwa karibu sana.

Kazi ya karama ya neno la hekima na inavyofanya kazi:
1. kukupa jibu la swali unaloulizwa lakini hasa swali lenye hila, mtego, ushindani au mashtaka ndani yake.
Luka 21:12-15 inasema ”lakini, kabla hayo yote hayajatokea watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi…….. basi kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza, mtakavyojibu, kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga”.
Luka 20:19-26; ”…lakini yeye alitambua hila yao …..”
Marko 3:1-6; inasema ”……….akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza simama katikati ……….nyosha mkono wako. Naye akaunyosha mkono wake ukawa mzima tena”.
Hapa tunaona neno la maarifa (kutambua hila ya wale waliotaka kumkamata) ilianza kufanya kazi, neno la hekima pia likafanya kazi baadaye pale Yesu alipomwambia yule mwenye kupooza ”simama katikati” na tunasoma akaanza kuzungumza na wale watu.

2. inakupa uwezo wa kutatua tatizo lililoko mbele yako.
Mathayo sura ya 1 na ya 2: Habari ya Yusufu na Mariamu. Katika sura hizi karama ya neno la maarifa na la hekima ilifanya kazi kwa kutumia ndoto. Si ndoto zote zinatoka kwa Mungu lakini kama ukiwa na neno la Mungu utatambua ndoto ya Mungu na isiyo ya Mungu.

3. kukupa uhuru wa kushirikiana na watu usiowajua kwa kazi ya Mungu.
Matendo ya mitume 10:1-20; Habari za Petro na Kornelio. Habari hii inaeleza jinsi Petro alivyoona maono wakati amezimia roho (akili zake zilikuwa hazina matunda).
Maono ya aina nyingine, kama tulivyokwishaona hapo nyuma ni ya wazi, ambapo akili zako zinaona na zinaelewa na bado unaweza kuona katika ulimwengu wa roho.
Aina nyingine ni maono ya ndani kwa mfano: unapoomba halafu ghafla ndani yako inakuja picha.
Sasa karama ya neno la maarifa na la hekima itakusaidia kukuwezesha kushirikiana na watu usiowajua.

4. inakurahisishia kuamua kwa haki katika nafasi ya uongozi Mungu aliyokupa au mahali unapohitajika kutoa maamuzi
I Wafalme 3:4-28; habari za mfalme Sulemani, jinsi alivyoomba hekima kwa Mungu na akapewa. Vilevile tunaona jinsi ambavyo aliweza kutoa uamuzi wa haki juu ya kesi ya wanawake wawili waliokuwa wakigombea mtoto. Uamuzi wa haki unahitaji msaada wa Mungu.

SEHEMU YA SITA
Karama ya unabii
I Wakorintho 12:4,10 ”Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule. na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii, na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha.
I Wakorintho 14:12; inasema ”…….takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa”.
Mambo ya msingi kuhusu huduma ya Nabii na karama ya unabii:-
1. kuna tofauti kati ya huduma ya nabii na karama ya unabii.
Efeso 4:11 ”Naye alitoa wengine kuwa Mitume; na wengine kuwa manabii….”. Hapa anazungumza habari ya nabii (ofisi) ya nabii. Huduma ni ofisi na karama ni vitendea kazi katika ofisi.

Kazi za nabii (kama huduma)

kufundisha mafundisho ya msingi / ya kuweka msingi wa kiroho ndani yako. Efeso 2:19-20 inasema, ”Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, ……..mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni”. Hii haimaanishi kwamba kila nabii amepewa kufundisha.

 Nabii pia anaweza kupewa kufanya kazi ya kubomoa na kuharibu kazi za shetani na kupanda pando la Mungu ndani ya mioyo ya watu, kama kuna mahali panahitajika kufanya hivyo. Tunaweza kusoma haya katika kitabu cha Yeremia 1:4,5,10; inasema ” …..kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa …………. Ili kung’oa na kubomoa na kuharibu na kuangamiza; ili kujenga na kupanda”.

Kazi nyingine ni kuonya. Tunaweza kuona haya katika kitabu cha Ezekieli 2:3-5; ”akaniambia mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israel, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi wao na baba zao wamekosa juu yangu…..”

Kazi nyingine ni mwonaji. I Samweli 9:9 ”(Hapo zamani katika Israel, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa mwonaji)”.

 Kutabiri (kusema mambo yajayo). Yeremia 23:21; inasema ”mimi sikuwatuma manabii hao, lakini walikwenda mbio; sikusema nao, lakini walitabiri.

Kazi ya karama ya unabii. (kama kitendea kazi):
Ni kujenga, kufariji, kutia moyo na kujirunza, pia huthibitisha kile ambacho Mungu amekwisha kusema na wewe. Katika kitabu cha I Wakorintho 14:3,4,24,25,31; tunasoma ”Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo. Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali ahutubuye hulijenga kanisa. Lakini wote wakihutubu, kisha akaingia mtu asiyeamini, au mjinga, abainishwa na wote, ahukumiwa na wote; siri za moyo wake huwa wazi, na hivyo atamwabudu Mungu, akianguka kifudi-fudi, na kukiri ya kuwa Mungu yu kati yenu bila shaka. Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja, ili wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe”.

2. manabii wapo hata leo ila nafasi zao ni tofauti na za wale wa agano la kale.
Efeso 4:11,14; ”naye alitoa wengine kuwa mitume na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamisisha watakatifu; hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa Imani na kumfahamu sana mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu…………. Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja tukizifuata njia za udanganyifu”.
Pia katika kitabu cha Matendo ya Mitume 13:1; tunasoma ”……. Palikuwako manabii na waalimu …..”. hii inaonyesha kuwa manabii wapo hata leo.
Tofauti iko hivi: kwamba manabii hapo zamani (katika agano la kale) walikuwa viongozi wakiongoza watu, yaani walipewa kuongoza watu, lakini katika agano jipya huduma ya nabii ipo ndani ya Kanisa na nabii hakupewa kuongoza kanisa- kila mmoja wakati huu amepewa Roho Mtakatifu ambaye anamwongoza. Hivyo nabii anayesema kwa mausia ya Mungu ni yule anayesema sawasawa na neno la Mungu.

Kanisa linajengwa juu ya misingi miwili ambayo ni:
a. Yesu Kristo
b. Mafundisho ya mitume na manabii ambao wanafundisha mafundisho ya msingi ambayo yanamfanya mtu awe mkristo. (foundation series). Ukisoma kitabu cha Waebrania 6:1; inasema ”kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundishao ya kwanza ya Kristo; tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na Imani kwa Mungu na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu na hukumu ya milele”.

Manabii wa sasa wanatofauti na akina Paulo na akina Petro ambapo hao wa zamani walipewa mafundisho ya msingi na hawa wa sasa wanapewa wito (hekima au special revelation) wanaposoma Biblia wanafungua siri za mafundisho ya msingi, ambayo akina Paulo walifundisha, na kutufunulia sisi.

Watumie rafiki zako kupitia;

  • Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Share on X (Opens in new window) X
  • Share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Email a link to a friend (Opens in new window) Email
Like Loading...

Mwl. Christopher Mwakasege; Zijue Karama Za Roho Mtakatifu – I

Posted by Gospel News Media on August 15, 2012
Posted in: Mafundisho. 1 Comment

Mwl. Christopher Mwakasege

I Wakorintho 14:12. Inasema ‘vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za rohoni, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa. Mungu hafanyi kitu bila kusudi, na kusudi la semina hii ni:-

Kuna jambo Mungu anataka kufundisha katikati yetu ambalo litahusisha sana utendaji wa karama za Roho Mtakatifu.

 Kurahisisha ujenzi wa kanisa lake na kazi zake. Mfano, kuna urahisi wa kujenga kwa kutumia mashine za kujengea na kubeba matofali kuliko kutumia mkono, ni sawa na kufanya kazi ya Mungu kwa kutumia karama za Roho Mtakatifu.
I Wakorintho 12:4; anasema pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule. Karama si za mtu ni za Roho Mtakatifu na kazi yake ni kulijenga kanisa.

Yesu alisema katika kitabu cha Mathayo 16:18; ”nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitaliweza”. Karama zinatokea mahali kama apendavyo Roho. Katika kitabu cha Yohana 14:16, Yesu alizungumza habari za kutuletea msaidizi mwingine, yaani Roho atakapokuja atachukua nafasi ya Yesu katika kulijenga kanisa lake.
Roho Mtakatifu sio karama bali anazo karama, pia Roho Mtakatifu sio nguvu bali anazo nguvu. Tunda la Roho linapofunuliwa ndani ya mtu tabia ya Mungu hujitokeza kwake.

Katika kutafuta vitu vya Mungu, ili kufahamu karama za Roho Mtakatifu na kazi zake, kuna gharama. Mfano, kwenye ndege kuna first class, business class na third class. Ukitaka kupata huduma nzuri zaidi lazima uongeze pesa (gharama) ili upande business class au first class. Lakini dereva wa ndege (captain) ni yule yule. Vivyo hivyo katika maswala ya Mungu wako wanaokaa first, business au third class, lakini wote tunakwenda mbinguni. Hivyo tunahitaji kuingia gharama ili tukae first class ndani ya Yesu. Gharama hizo ni kama:-
i) kusoma neno la Mungu kwa bidii kwa kadri inavyowezekana ili neno hilo likae ndani yako kwa wingi, maan kujua karama za Roho Mtakatifu bila kuwa an maneno ya Mungu ni vigumu.
ii) Maombi n.k.

I Wakorintho 12:1 inasema ‘basi ndugu zangu kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu’. Tunahitaji kuwa na hamu ya kuona kwamba karama za Roho Mtakatifu zinafanya kazi na zinafahamika. Hamu hiyo imepotea katika kanisa la Mungu na hivyo kufanya kazi ya ujenzi wa kanisa la Mungu kutofanyika kama Mungu anavyokusudia.

I Wakorintho 14:12; ”Vivyo hivyo na ninyi kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa”.

UTENDAJI KAZI WA KARAMA.
Mambo muhimu (ya msingi) kufahamu ili karama ziweze kufanya kazi. Mambo hayo ni:-
1.) Kubali kuwa karama za Roho zinaweza kufanya kazi kwako pia.

I Wakorintho 12:4.11; ”Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule, lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye”. Roho Mtakatifu ndani ya mtu anazo karama zote bali anamgawia kila mtu kama apendavyo yeye. Rumi 12:3-6; inasema ”kwa maana kwa neema niliyopewa na mwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyo mpasa kunia ……….., basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali …………..”.

2.) Uwe na hamu (haja) kubwa ya msaada wa Mungu.

I Wakorintho:1,12; ”ufuateni upendo na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu, vivyo hivyo na ninyi kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa”.
Angalizo: karama siku zote zina mvuto.

3.) Tembea katika wito (nafasi) yako.

Warumi 12:6, ”……… kwa kadri ya neema tuliyopewa…”, yaani wito (kiwango) ulichopewa. Ndani ya wito kuwa nafasi ambayo Mungu amekupa. Kuna ngazi, kuna mahali na muda unaotakiwa kuufanyia huo wito. Galatia 2:6-7 ”……walipokwisha kujua neema niliyopewa…….. walinipa mimi mkono wa kuume wa shirika”.
Mfano: kuna tofauti ya karama ya unabii na huduma ya unabii, yaani kila mtu aliyeokoka anaweza kutoa unabii bali si kila mtu ana karama ya unabii.

4.) Karama kutenda kazi vizuri ndani ya mtu inategemea kiwango cha Imani alichonacho.

Rumi 12:6; ”basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali …….. ikiwa unabii tutoe unabii kwa kadri ya imani”. Sio zaidi ya hapo. Rumi 10:17; ”imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo” yaani kiwango cha imani ulichonacho hakiwezi kuzidi hapo. Imani huja tu kwa neno la Kristo. Biblia haituruhusu kutembea kwenye karama zaidi ya imani tuliyo nayo.
Angalizo: kufahamu neno la Kristo kwa wingi ni muhimu. Tembea katika karama za roho kwa kadri ya imani.

Karama zitumike kwa kadri ya Imani yaani utendaji kazi wa karama za Roho Mtakatifu ndani ya mtu utategemea kiwango cha neno la kristo kilichoko ndani yake. Hii ni kwa sababu Mungu alikusudia kuwa karama katikati ya kanisa zifanye kazi kwa ufanisi na usalama ili kulijenga kanisa.
Mfano: Mungu hakuweka unabii ili uongoze kanisa; ila ni kwa ajili ya kuthibitisha neno ambalo Mungu amekwisha kulisema ndani ya mtu.
Kwa sababu karama si zako ni za Roho Mtakatifu, kama huna neno la kutosha ndani yako karama inaweza ikaletwa ndani yako ukaikataa.

I Wakorintho 12:8 ”maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa apendavyo Roho yeye yule”. I Petro 4:10; ”kila mmoja kwa kadri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana….”. Kuna kupewa na kupokea- karama. Unaweza kukataa kwa kutokuja au hofu n.k.

5.) Jifunze jinsi Roho anavyowasiliana na roho yako, nafsi yako na mwili wako.

I Wakorintho 3:16; ”hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?” Mtu ni roho anayo nafsi na anaishi katika mwili. Roho Mtakatifu pia yuko ndani ya mwili. Hesabu 30:2 ”Mtu atakapo mwekea Bwana nadhiri, ……. Asitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake”. Unaposema maneno yanafunga nafsi yako.

Mwili unatawaliwa na nafsi, nafsi kazi yake ni kutafsiri kile ambacho mwili unasema ili roho ielewe na kile ambacho roho inasema ili mwili uelewe. Kwa hiyo nafsi inasaidiwa pale, unaposoma neno ili iweze kutafsiri mambo ya rohoni sawasawa na neno. Marko 2:5-8, ”naye Yesu, alipoiona imani yao, …….. wakifikiri mioyoni mwao ….. Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao …..”. Galatia 6:17; ”tangu sasa mtu asinitaabishe kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.

6.) Ujazo wa Roho Mtakatifu. Sio wa siku moja ambao unatosheleza.

I Petro 4:9-11 ”mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika, kila mmoja kwa kadri alivyoipokea karama,……….. mtu akihudumu na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu, …….”. yaani kila wakati kuna nguvu fresh, mtu asihudumu kwa nguvu alizojaliwa bali anazojaliwa kila wakati na Mungu. Hivyo tunahitaji kurudi kwa Mungu kila wakati kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu.
Kuna kiwango cha nguvu za Roho Mtakatifu ndani ya mtu ambacho hakiwezi (kwa kuwa ni kidogo) kusukuma karama fulani ili ziweze kuhudumu au kufanya kazi; ndio maana tunahitaji kujazwa kila wakati.

Usikose Sehemu ya Muendelezo wa Somo hili Siku ya Kesho.

Watumie rafiki zako kupitia;

  • Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Share on X (Opens in new window) X
  • Share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Email a link to a friend (Opens in new window) Email
Like Loading...

SIMULIZI: Nilikula Nyama za ndugu wa damu 19 (Sehemu ya Tatu).

Posted by Gospel News Media on August 14, 2012
Posted in: Simulizi. 2 Comments

Inaendelea……………………………………………

Baada ya muda mfupi nilipoteza fahamu zangu kabibsaaaa, na nilikuja kushtuka nikiwa chumbani kwangu. Tofauti na Siku zingine, siku hiyo nilichelewa sana kuamka na niliamka nikiwa mchovu sana. Nakumbuka ilikuwa ni kama mida ya Saa 7 mchana, na hata Bibi hakuniamsha siku hiyo mpaka nilipoamka mwenyewe.

Kabla Sijatoka nje, gafla nikakuta Bibi anaingia Chumbani kwangu. “Esther hujambo?” Alinisalimu Bibi, nikamjibu sijambo na kisha nikamuamkia. Kwakuwa bado nilikuwa na kumbukumbu na tukio zima la jana usiku, nikaanza kumuuliza Bibi, “Kwani Bibi Jana usiku tulikuwa wapi?”. Bibi akasema kwa nini unaniuliza hivyo? Nikamwambia naona mwili wangu umechoka sana na nakumbuka tulitoka hapa usiku tukaelekea sehemu flani hivi ila sikujui ni wapi, na mashavu yananiuma sana.

Kwa kukwepa kunambia ukweli Bibi akaanza kunambia kuwa Niliumwa sana jana usiku na kuzidiwa jambo lililomfanya Bibi kunipeleka kwa mganga. Jibu lake sikulielewa kutokana na mfululizo wa matukio ninaoukumbuka mimi, jambo hili lilinifanya nimuulize Bibi swali lingine, “Kwani Bibi …………” Kabla sijamaliza kumuuliza swali hilo, Bibi akanikatisha, “Wewe nimechoka na maswali yako, hebu nyanyuka uende kuoga, na usimwambie chochote babu yako kuhusu jambo hili, kama akikuuliza kwanini umechelewa kuamka Mwambie ulikuwa hujisikii vizuri, sawa?” Nikamjibu Sawa. Niliamka na kwenda kuoga.

Usiku uliofuata sikupata usingizi kabsaaaaaaa, kutokana na tukio la jana usiku. Na hili lilichangiwa na mimi kulala peke yangu. Niliogopa sana kwakweli na hapa nilishaanza kuamini kwa kiasi flani kwamba Bibi yangu ni Mchawi.

Muda ulizidi kwenda, na katikati ua Usiku nikianza kupata pata usingizi Bibi aliingia Chumbani kwangu kwa kupitia pale pale kwenye ile kona ya Chumba changu akiwa na mavazi kama ya jana usiku. Gafla nilinyanyuka pale kitandani na kujikuta nikianza kulia huku nikimwambia kuwa staki kwenda. Bibi alianza kunibembeleza kuwa leo nitafurahi mwenyewe mana sitapigwa na kuna kitu kizuri wameniandalia.

Sikutaka kumuelewa mambo aliyokuwa akiniambia hivyo nilizidi kulia huku nikiendelea kumwambia kuwa staki kwenda. Majibu yangu yalimpa hasira sana, na kama kawaida yake alichukua madawa yake na kupaka usoni. Pale pale ujasiri uliniisha na nilikuja kushtuka nikiwa kule kule tulipokuwa Jana usiku.

Leo hii kilikuwa ni siku ya Kikao. Kikao ambacho kiliwekwa maalum kwa ajili ya kunikaribisha kwenye kundi lile la Wachawi. Kwa utaratibu waliokuwa wamejiwekea ni kwamba, kila mtu mpya anayejiunga kwenye kundi lile basi ni lazma amtoe kafara ndugu yake 1 wa karibu ili kundi zima la wachawi tumle.

Shughuli ya kumpendekeza mtu huyo huwa ni ya mwenye ndugu hivyo wakanipa nafasi ya Mimi kumtaja ndugu yangu wa karibu ambae nataka wachawi wale wamle. Asikwambie mt, siku ile nilitamani ardhi ipasuke na nitumbukie ndani ili nisiweze kufanya Jambo hilo. Nilianza kuhisi jasho jembamba likinitiririka usoni huku nikiwa natetemeka kwa dhambi wanayotaka niitende.

Je! Nini kitaendelea? Esther atakubali kufanya hivyo? Na kama atakubali, atampendekeza nani? Usikose Muendelezo wa simulizi hii ya kusisimua ili uone ni namna gani nguvu ya Mungu inavyofanya Kazi.

Watumie rafiki zako kupitia;

  • Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Share on X (Opens in new window) X
  • Share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Email a link to a friend (Opens in new window) Email
Like Loading...

Elder Daniel Akakpo (COP Mass Choir) – Jehovah You are the most High

Posted by Gospel News Media on August 14, 2012
Posted in: Nyimbo Mbalimbali. Leave a comment

Watumie rafiki zako kupitia;

  • Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Share on X (Opens in new window) X
  • Share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Email a link to a friend (Opens in new window) Email
Like Loading...

Posts navigation

← Older Entries
  • Join Us now on Facebook

    Join Us now on Facebook
  • New Albam Ya Jessica Honore

    Jessica's New Album is Comming Soon!!!

  • UNIVERSITIES’ UPDATES – TZ

    *********************************************************

    UKWATA TANZANIA (MIKOA YOTE)
    Kusanyiko la Viongozi wa UKWATA - TAIFA ambalo huwa linafanyika Kila Mwaka katika Mikoa tofauti tofauti, Mwaka huu Kusanyiko hilo litafanyika katika Mkoa wa Mwanza Kuanzia August 8 - 13. Lengo ni kukutana pamoja na kushirikishana mipango mbalimbali ya Ukwata Kitaifa.

    **********************************************************

    TANZANIA THISDASO - ECD RETREAT
    This year's ECD Retreat(2012) will be hosted in Kampala Uganda, at
    Bugema University, from 19th-26th Dec, 2012. The ECD retreat involves about 9 countries in East and Central Africa division. Other neccesary information about the 2012 ECD retreat will be regularly updated to our website; www.thisdaso.org

  • ALBAM MPYA ZA HIVI KARIBUNI

    Audio Albam ya Mwimbaji Noel Didas ya "Uniinue Viwango Vingine" yenye Jumla ya Nyimbo 10, sasa unaweza kuipata kwa Kuwasiliana nae kupitia Nambari; 0655 115990 au 0765 115990

  • Calender of The Year 2012

    September 2026
    M T W T F S S
     123456
    78910111213
    14151617181920
    21222324252627
    282930  
    « Sep    
  • Our Recent Posts

    • Kuhama kwa Blog Hii.
    • Mchungaji Kanisa la Gospel Campaign Centre, Azindua Operation maalum ya wiki tano ya Maombezi na Uponyaji.
    • The Holy Bass Guitar Concert with James Honore in Dar es saalam.
    • Faustin Munishi kuhubiri Injili Nchini Congo Mwezi huu.
    • SIMULIZI: Nilikula Nyama za ndugu zangu wa damu 19 (Sehemu ya Nne).
    • Kanisa la EAGT Tarime ladaiwa kuuziwa Kiwanja cha Serikali kinyemela.
    • Mwl. Christopher Mwakasege; Zijue Karama Za Roho Mtakatifu – II
    • Mwl. Christopher Mwakasege; Zijue Karama Za Roho Mtakatifu – I
    • SIMULIZI: Nilikula Nyama za ndugu wa damu 19 (Sehemu ya Tatu).
    • Elder Daniel Akakpo (COP Mass Choir) – Jehovah You are the most High
  • Our Blog Archives

    • September 2012
    • August 2012
    • July 2012
    • June 2012
    • May 2012
    • April 2012
    • March 2012
    • February 2012
    • January 2012
  • Taarifa katika Makundi

    • Cartoon's Stage
    • Habari
    • Jicho la Tofauti
    • Mafundisho
    • Matangazo
    • Matukio
    • Mistari ya Nyimbo
    • Nyimbo Mbalimbali
    • Simulizi
    • Teachings
    • Tenzi Za Rohoni
    • Waimbaji Wetu
  • Andika E-mail yako hapa

    Join 63 other subscribers
  • Blogs za Kikristo

    • Erick Brighton Blog
    • Gospel Kitaa
    • Hosanna Inc
    • John Shabani
    • Patrick Sanga Ministry
    • Rumafrica
    • Sam Papaa
    • Strictly Gospel
    • Uncle Jimmy
    • Vipaji Halisi
    • Women of Christ
  • Tovuti za Kikristo

    • Believers Ministry
    • Mwl. Christopher Mwakasege
    • Pastor Dr. Daniel Kulola
  • Soma Magazeti Haya

    • Gazeti la Daily News
    • Gazeti la Habari Leo
    • Gazeti la Mwanahalisi
    • Gazeti la Mwananchi
    • Gazeti la Mzalendo
  • Blog ya Simulizi

    • SIMULIZItz
  • Ruth Lyanga George

  • Adolph Robert Nzwalla

  • Christina Shusho

  • Samwel Batenzi a.k.a Dube

  • Dar es salaam Gospel Team

  • Sikiliza Hhc Alive Fm Online

  • Sikiliza Wapo Radio Fm Online

  • You are a Visitor Number

    • 406,908
  • Our Online Visitors

  • Kwa Habari Mbalimbali, Join

    Kwa Habari Mbalimbali, Join
  • Search

Create a free website or blog at WordPress.com.
Gospel News Media
Create a free website or blog at WordPress.com.
Privacy & Cookies: This site uses cookies. By continuing to use this website, you agree to their use.
To find out more, including how to control cookies, see here: Cookie Policy
  • Subscribe Subscribed
    • Gospel News Media
    • Join 63 other subscribers
    • Already have a WordPress.com account? Log in now.
    • Gospel News Media
    • Subscribe Subscribed
    • Sign up
    • Log in
    • Report this content
    • View site in Reader
    • Manage subscriptions
    • Collapse this bar
Loading Comments...
%d
    Design a site like this with WordPress.com
    Get started